0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wanafunzi wa Sekondari mara baada ya kuhutubia wakazi wa Sengerema vijijini wakati akielekea kuzindua mradi wa Maji.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mwenyekiti wa Kamati ya amani ya Mkoa wa Mwanza Sheikh Hassan Kabeke mara baada ya kufungua mradi huo wa maji.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi wengine akifungua mradi mkubwa wa maji katika kijiji cha Nyamazugo Wilayani Sengerema. Mradi huo unatarajiwa kuhudumia wakazi wa Sengereza kwa asilimia 100 tofauti na asilimia 33 ya awali Julai 4, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mwanachama mpya wa CCM ambaye alikuwa Kada maarufu wa CHADEMA kanda ya Ziwa Hamis Tabasamu wakati akihutubia wakazi wa Sengerema mara mara baada ya kuzindua mradi mkubwa wa maji katika kijiji cha Nyamazugo, Sengerema mkoani Mwanza.

 

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top