0
HOFU  imetanda kuhusu mkutano wa Bunge unaotarajia kuanza kesho kwamba unaweza kutekwa na sakata la kukamatwa ndege ya serikali aina ya Bombadier
Wabunge wa  Chama Cha Mapinduzi (CCM), wameanza kuingiwa na hofu na kwamba kuna uwezekano wabunge wa upinzani wakaibuka na kutaka majibu ya serikali kuhusu sakata la ndege hiyo.
Wakizungumza kwa mashariti ya kutokutajwa majina wabunge hao wa CCM wamesema  kama Spika wa Bunge, Naibu Spika au wenyeviti hawatakuwa wakali kuzuia hoja hizo Bunge linaweza kuwaka moto.
Baadhi ya wabunge kutoka mikoa ya kanda ya ziwa wamesema kuwa awali wawakilishi hao walisifu kitendo cha rais John Magufuli kuzui mchanga wa makenikia lakini hili la  Bombadier linaweza kuleta shida.
Wamesema Bunge linaweza kutawaliwa na mijadala ambayo inaweza kutokana na upinzani kutaka majibu ya haraka kuhusu sakata la Makinikia, kikao cha majadiliano na wawakilishi wa kampuni ya Barrick waliokuja nchini kuzungumza na sekali pamoja na ndege ya Bombadier.
Amesema kwa sasa wabunge wengi wa CCM ni kama wameisha kata tamaa ya kuendelea kumtetea rais kwa kuwa mambo mengi ambayo yanaibuliwa na wapinzani mengi yanaonekana kuwa ni ya kweli licha ya kupindisha ukweli.
“Kwanza kwa sasa tumeisha tofautiana wabunge wengi hatuana kauli moja wabunge wengine wamekuwa waoga kuongea ukweli kilichobaki ni kulalamikiana,” amesema
Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema) amesema Bunge linaloanza kesho kuna uwezekana likatawaliwa na hoja ambazo zinalenga kujua mstakabari wa taifa.
Kubenea ametoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kutoka mahakamani ambapo anakabiliwa na kesi ya kudaiwa kumshambulia mbunge mwenziwe wa CCM.
Hivi karibuni mwanasheria mkuu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu  amesema ataingia bungeni na hoja mbalimbali ikiwamo hiyo ya kukamatwa ndege ya serikali nchini Canada.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top