0

Image result for mgodi wa chumvi manyaraHalmashauri ya Wilaya ya Hanang’ iliyopo mkoani Manyara imefanikiwa  kutatua mgogoro uliokuwa ukiendelea kati yao na  wizara ya nishati na madini  kanda ya kasikazini uliokuwa ukihusiana na utozwaji wa ushuru katika  mgodi wa chumvi uliopo katika kata ya  Gendabi  wilayani humo.
 Akizungumza katika mkutano na wakazi wa  vijiji vya Gendabi,Sebasi,Hargushay na Sarjanda  vyote vikiwa vinaunda kata ya Gendabi Kamishina msaidizi wa  wizara ya nishati na  madini kanda ya kasikazini Bw.Adam Juma alieleza kuwa mgogoro huo ulitokana  na fedha zilizokuwa   zikitolewa na serikali  kwa ajili ya kusaidia vikundi vidogo vidogo vya wachimbaji wa madini  kwa ajili ya  kuwakwamua   na kuwapa ari ya  kufanya kazi.
 Jumla ya    vikundi 59  vilivyosajiliwa nchini  hapa vimenufaika na fedha hizo za serikali huku mkoa Wa manyara ukijwa kuwa na vikundi 6 ambapo  kukindi  kimojawapo ni cha uchimbaji wa chumvi katika mgondi wa chumvi  wa Hargushay kinachofahamika kwa majina ya Hasami  kinachochimba chmvi katika mgondi huo pamoja na kuuza.
 Mgodi wa Hargushay unaelezwa kuwa na vikundi viwili ambavyo ni  Gesami na Hasami lakini ikaelezwa kuwa  kikundi kilichosajiliwa ni hasami  na ndicho kinatakiwa kupata fedha hizo  jumla ya million 90 ambapo kwa pande mwingine kulitokea kutoelewana kati ya vikundi hivyo huku wote wakidai wapo kihalali bila kujali kama hwajasajiliwa.
 Naye mkuu wa wilaya  ya Hanang’ Sarah Msafiri  alieleza chumvi inazalishwa katika mgondi huo imekuwa ikisafirishwa kwenda nchi za Rwanda,Burundi,Kenya  na Malawi  kwa ajili ya matumizi mabalimbali lakini mafanikio  ni kdogo ikilinganishwa na uchimbaji unaofanywa katika mgondi huo na hiyo ni kutokana na  kukosa usimamizi wa kukusanya mapato katika njia zilizosahihi hivyo kuisababishia hasara halmashauri na hata wao wenyewe kutokana na kufanya uuzaji holela.
‘’Ndugu zangu  tumekuja hapa leo ili tumalize mgogoro uliokuwa ukiendelea hapa na kusababisha  magari yanayosafirisha  na kununua  chumvi kusimamishwa kwa madai kuwa hawaruhusiwi kusafirisha mpaka wapate kibali cha mamlaka ya hali ya hewa [TMA] ndipo waweze kusafirisha lakini leo tumemaliza suala hilo  na Kamshina wetu na sasa wasafirishaji na wanunuzi watafanya kazi hiyo kama ilivyokuwa siku zote’’alisema Bi. Sarah.
Awali kabla ya mgodi huo kuwa chini ya halmashauri ulielezwa kukusanya kwa mwaka jumla ya  Million 19 kwa mwaka ambazo wanakikundi walikuwa wakigawana  lakini badala ya Halmashauri hiyo kugundua inakosa   mapato makubwa katika  Mgondi huo waliamaua kupeleka mashine za EFD’s kwa ajili ya ukusanyaji  Ushuru wa mapato yanayotokana na  uuzaji wa chumvi hiyo na walifanikiwa  kukusanya jumla ya Million 117 kwa  mwaka.
 ‘’ Kwa kuwa tumekubaliana na kamishna kwa sasa tutaendelea kutumia mashine  hizi  ambapo makato yatakuwa ya moja kwa moja ya  ushuru kwenye mashine ile kutakuwa na ushuru wa  Wizara ya  madini  ambao utakuwa unakatwa moja kwa moja na  sisi halmashauri tutakata  fedha yetu ya ushuru haya ndio makubaliano yetu na nafikiri  kama tu tumefanya usimamizi mzuri na tukakusanya million 117  na ukiangalia ukubwa wa mgondi wetu unaturuhusu kupata fedha zaidi ya hiyo  ila usimamizi ndio haukuwa sawa  ila kwa sasa  tayari  tumemuweka mkusanya ushuru ili tusipoteze tena mapato ‘’ alisema Bi. Sarah.
Madini hayo aina ya chumvi  katika mgodi wa Hargushay yameelezwa kupatikana kwa msimu ambapo inakuwa ni kiangazi na wakati wa kipindi cha masika maji hujaa ivyo huwalazima kusubiri maji yakauke ndio  waweze kuvuna chumvi lakini mkuu wa wilaya akawahakikishia endapo kutakuwa na usimamizi bora utaohusisha wataalamu chumvi hiyo itavunwa  muda wote  na syo kwa msimu.
 Naye mkurugenzi mtendaji wa wilaya    ya Hanang’ Bryceson Kibassa alieleza  mradi huo haujatumiwa vizuri ili kuwanufaisha wananchi wa vijiji hiyo na kubadili maisha yao  kutokana na mgondi ho kuwa na  mgogoro kati yao wanavjiji k na chumvi kuzalishwa kwa  kiasi kikubwa na kuuzwa kwa bei ya chini ambapo kwa sasa ngunia linauzwa kwa Tsh 1000.
 Aidha alieleza kuwa kinachotakiwa ni kuendelea kuweka kiwango  cha juu kcha uuzaji wa chumvi paoja kuboresha bora wa chumvi hiyo  ili kuweza kupata masoko ya uhakika  na yatakayowanuisha wazalishaji wa  chumvi.
Ayubu Ramadhani  ni  msafirishaji wa chumvi ni mmoja kati ya wasafirishaji ambao magari yao yalisitishwa kusafirisha chumvi kutoka mgodi wa Hargushay  ambaye anapeleka chumvi hiyo Nairobi  alieleza kuwa ni miaka miwili sasa toka ajiingize kwenye biashara ya  chumvi  lakini hali bado haijabadilika licha ya wao kutoa ushuru halmashaur kwani miundo mbinu ya  barabara  hiyo ina makorogo  haina galavati  hivyo imekosa hadhi ya kusafishia  magari ya mizingo mikubwa na mizito hivyo waliomba serikali  kuwaboreshea barabara  ili waweze kusafirisha kiurahisi.
 Chumvi ya  Gendabi inaelezwa kuuzwa nchi za nje  kwa ajili ya kukaushia ngozi, kubadilishana chumvi na mahindi au vitu vingne na nyingine hutumika kwa matumizi ya kawaida ya kupikia.
Wakazi wa kata hiyo waliomba kuboreshewa  soko la chumvi hiyo ambayo imeonekana kushuka kwa kiasi kikubwa  kutoka elf tatu waliyokuwa wakiuza  kwa mwaka jana  mpaka kufikia elfu 1000 ambayo imekuwa ni kidogo na kushindwa kuwasaidia kwa kiasi kikubwa kwani wengi hutengemea kuuza chumvi kwa ajili ya kupata fedha ya matumizi pamoja na kuwasomeshea watoto wao.
 Aidha  mkuu wa wilaya amewataka  wananchi wa vijiji hivyo kuendelea kujiunga na vikundi ikiwa ni pamoja na kuanzisha vikundi vipya na kuvisajili ili viweze kupata leseni  na kunufaika na fedha za seikali huku akieleza kuwa lengo ni kufikia vikundi 100 vya ujimbaji chumvi katika mgodi huo.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top