0


Binti wa miaka 22 aliejifungua mapacha watatu wote wa jinsia ya kike wilayani Babati mkoani Manyara  na kukimbiwa na mume wake,anaomba msaada kwa wasamaria wema ili aweze kuwalea watoto hao.
Ambae yupo tayari kumsaidia mama huyo, anaweza kumsaidia kupitia   namba za simu ni 0766 32 02 42.
Leonika Andrea Ni binti mwenye miaka 22 anaeishi katika kijiji cha Managha kata ya Singe Halmashauri ya mji wa Babati mkoani Manyara,alihitimu elimu ya Sekondari  kidato cha nne mwaka 2013  katika shule ya Sekondari Sumaye.
Alibeba mimba ya pili akiwa na mwanaume wake Sigifridi  motto wa kike waliompatian jina la Caren,mara baada ya kubeba ujauzito wa pili mwaka 2016 alikuwa na mahusiano mazuri na huyo mwanaume wake,siku zikazidi kwenda Leonika Mungu akamsaidia akajifungua mapacha watatu katika hospitali ya mji wa Babati Mrara ambao walikuwa na kilo moja moja hivyo kulazimika kuhifadhiwa katika  chumba maalumu  cha joto  katika hospitali hiyo mpaka walipoongezeka uzito na hatimaye kuruhusiwa kurejea nyumbani.
Leonika anaishi na mama yake ambaye ni mkulima na mfugaji,baba ameikimbia familia tangu mwaka 2011 ana aliaga anakwenda mjini Dodoma kutafuta Maisha lakini mpaka sasa hajaonekana nyumbani na pindi anaporejea nyumbani ,haji na chochote kama ilivyozoeleka kwamba baba anaporejea lazima aje na kitu amabacho kitaifurahisha familia.
Mama wa mapacha watatu Leonika Andrea anasema walikutana na mwanaume huyo Rombo Kilimanjaro na wakakubaliana na kuishi pamoja na kupata mtoto wa kwanza ,lakini baada ya kujifungua mapacha watatu mwanaume alibadilika na kurudi kumuiba mtoto wao wa kwanza ambaye ni Carren na mpaka sasa hajui alipo na namba ya simu kabadilisha.
Mama Leokania anasema kuwa anashindwa hata kufanya vibarua kwa ajili ya kupata mkate wa kila siku kutokana na kuzidiwa na majukumu haswa ya kuywalea wajukuu hao kwani binti mwenyewe kwake inakuwa ni vigumu kwa watoto watatu.
Mama anaomba mwenye kuguswa na jambo hilo wajitolee kwa moyo chochote walichonacho ili wapte nguvu na kuendelea na shuguli nyingine.
Kwa upande wa majirani nao wamesema wametoa misaada yao kadri walivyoweza ila bado msaada unahitajika kwa ajili ya kuisaidia familia hiyo.
Msaada wako ni wa muhimu sana ili uweze kuwasidia watoto hao kuku vizuri,Kwa yeyote ambaye ataguswa kama binadamu anaweza kumsaidia Leonika kupitia  Mpesa namba za simu ni 0766 32 02 42
Wanasema leo kwake,kesho kwako. Mungu akubariki.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top