0

Image result for SARATANI YA SHINGO YA KIZAZIUtafiti unaonyesha kuwa Kila mwaka asilimia 27 ya watanzania hupoteza maisha  kutokana na magonjwa yasiyoambukiza yakiongoza magonjwa ya Sukari ,presha na saratani.
Hili ni ongezeko kubwa kwa mujibu wa takwimu za shirika la afya duniani.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa chama kinachopambana na magonjwa yasiyoambukiza [TANCDA]mkoani Manyara Nickodemus  Gaudence wakati wa kutoa  huduma za vipimo na matibabu bure katika Zahanati binafsi ya Margakan iliyopo Babati mjini.
Dk Nikocdemus ameiomba Serikali isaidiane na shirika la TANCDA ili kuondokana na matatizo haya yanayowakabili wengi haswa tatizo la uzuzi kwa wanawake.
Kutokana na kubainika kuwa ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi inachangiwa na ngono na mwanamke au mwanume ziadi ya mmoja  Dk Nickodemus ameshauri kuwa na  mwenza mmoja.
Shirikisho la vyama vya magonjwa yasiyo ya kuambukizwa Tanzania inayohusika na magonjwa yasiyoambukiza TANCDA kwa kushirikiana na Zahanati ya Margakan Tanzania tawi la Babati limetoa huduma za upimaji magonjwa bure
Nao wakina mama wameeleza kufurahishwa kwao na huduma hizo za vipimo bure vya magonjwa na kuitaka serikali ianzishe utaratibu huo ili kuwanusuru wakina mama na madhara yatokanayo na Saratani ya kizazi.
Kutokana na magonjwa hayo kutibiwa kwa gharama kubwa mfuko wa bima ya afya NHIF wamewataka wananchi kujiunga katika mfuko huo kwa kukata kadi ya matibabu na kuokoa kiasi kikubwa cha fedha za kutibiwa.
Charles Nyawaga yeye ni afisa wanachama mfuko wa bima ya afya mkoa wa Manyara anasema wameshatoa elimu juu ya umuhimu wa kuwa na kadi yua matibabu mkoa mzima na wanaendelea kuwashawishi wananchi kujiunga.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top