0

Image result for polisi wanawake tanzania MAZOEZIAliyekuwa Kamanda wa polisi mkoa wa Manyara Francis Jacob Masawe amewapongeza askari polisi wanawake   wa mkoa huu kwa kuonyesha uwezo mkubwa katika majukumu yao.
Kamanda Masawe ameayasema hayo wakati wa hafla ya kufunga  maadhimisho ya miaka 10 ya mtandao wa polisi wanawake Tanzania [TPF-NET]kwa mkoa wa Manyara yaliyofanyika mjini Babati katika hotel ya white Rose ambayo yalianza Oktoba 10 2017-14-2017.
Katika kipindi cha maazimisho hayo askari hao wanawake walitoa elimu kwa jamii ikiwemo mashuleni kupitia kitengo cha dawati la jinsia na watoto kwa wilaya zote tano ambapo jumla ya watu wazima 6,085,000 wamepata elimu kwa njia ya semina ,vikao huku watoto wapatao 405,000 wakipatiwa elimu kwa shule za msingi na sekondari.
Taasisi ambazo dawati la jinsia limeshirikiana mkoani Manyara ni World Vision,ustawi wa jamii wilaya na mkoa,Paralegal,Kanisa Katoliki jimbo la Mbulu,MAHOSE,NAFGEM,REDIO MANYARA pamoja na MWEDO.
Aidha  katika kuonyesha uwezo wao katika kazi,askari hao wa kike  walipangwa  sehemu mbalimbali za ulinzi kwenye mabenki ,kufanya mazoezi ya kivita,kulinda kituo huku wakiongozwa na Askari Insekta Pilly katika mazoezi.
Naye kamanda wa kikosi cha usalama Bara barani mkoa wa Manyara Mary Kipesha aliwataka askari hao wanawake wake za askari kushirikiana kwa pamoja katika kufichua vitndo vya kikatili vinavyofanywa katika jamii hata kama vinafanywa na askari wenyewe.
Askari hao wa kike katika risala yao kwa Kamanda Masawe wamesema kuwa yapo mengi wameyafanya katika kipindi cha maazimisho hayo huku wakisisitiza kuwa bado wana Ari ya kuchapa kazi kwa bidii na nidhamu ya hali ya juu kwa kuzingatia kuwa mtandao huo ni mojawapo ya maboresho ya jeshi la Polisi  hivyo wanaendelea kuchapa kazi huku wakiipigilia msumari kauli ya Rais John Pombe Magufuli ‘HAPA KAZI TU”.
 Mtandao wa polisi wanawake Tanzania ulianzishwa rasmi mwaka 2017 na aliyekuwa  IGP  Kipindi hicho  Said Mwema baada ya kuona  nchi zingine zina mtandao huo na zinafanya vizuri katika majukumu yao,na askari wote wanawake ni wanachama wa mtandao huo.
Mtandao huo ulianzishwa kwa madhumuni ya kuimarisha ulinzi na usalama wa watu na mali zao jambo ambalo ndio msiongi wa askari polisi kwa ujumla.
Mkoa wa Manyara una askari wanawake 232 kwa wilaya zote ambazo ni Babati,Mbulu,Hanang,Simanjiro na Kiteto.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top