0
Anaandika Sulleiman Ussi
Zanzibar


Image result for soka la ufukweni zanzibarKamati ya soka la ufukweni inaendelea vyema na maandalizi ya ligi kuu ya Zanzibar kwa upande wa soka ufukweni yanatarajia kuanza rasmi siku ya tarehe 4 mwezi wa 11.

Akitoa tamko hilo mwenyekiti wa soka la ufukweni Zanzibar Aliy sharifu ( Adofu ) mpaka sasa tayari uwanja umeshakaguliwa.

Ligi kuu ya Zanzibar kwa upande wa Soka la Ufukweni inatarajiwa kuanza rasmi Novemba 4, 2017 kwenye ufukwe wa Park Hyatt Shangani Mjini Unguja.

Amesema kamati yao wataanza kutoa fomu za usajili Oktoba 20 na Oktoba 25 ni siku ya kurejesha fomu hizo ili waanze ligi hiyo tarehe waliyoipanga.

“Matayarisho yanaendelea vizuri na ligi yetu tutaanza tarehe 4 mwezi wa 11, tayari tumeshatangaza tarehe ya kuchukua fomu za usajili na kurejesha, mwaka huu ligi yetu tutacheza kwenye fukwe ya Park Hyatt iliyopo Shangani”.

Wakati huo huo Adolf amevisisitiza vilabu kwenda kujisajili kwa mrajis wa vyama vya michezo Zanzibar na endapo kama havijasajiliwa hawatoweza kucheza ligi hiyo ambapo Oktoba 15 ndio siku ya mwisho kwenda kujisajili kwa mrajis.

“Navisisitiza vilabu viende kwa mrajis kujisajili na mwisho wa kwenda kwa mrajis ni Oktoba 15, mwaka huu kama timu haijasajiliwa na mrajis sisi hatutoipokea kwenye ligi yetu”. Alisisitiza Adolf.

 Mshauri mkuu wa soka hilo la ufukweni mzee Muhusin Aly Kamara Adolfu amesema katika msimu huu  ligi ya soka la ufukweni itachezwa saa 2 asubuhi kwa siku ya jumamosi na jumapili ya wiki hii. 
Wakati Soka la ufukweni likipigwa nayo ligi kuu ya Zanzibar kwa upande mpira wa miguu itachezwa jioni .

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top