0
Mkuu wa mkoa wa Manyara Dk. Joel Nkaya Bendera akimuuliza mtoa huduma wa MVIWATA kuhusu mafuta yaliyotokana na kitunguu Swaumu.
Suala la mbegu feki limekuwa likiwaliza wakulima wengi nchini hatua inayopigiwa kelele na  wakulima na wadau wa Kilimo.
Wakulima wamekuwa wakinunua mbegu ambazo zinakaa ardhini kwa muda mrefu bila kuota hali inayowafanya  wakulima wasiwaamini wauzaji wa mbegu hizo.
Mtandao wa wakulima mkoa wa Manyara [MVIWATA]wakiwa kwenye mkutano mkuu wa 10 katika ukumbi wa Hotel ya White Rose mjini Babati wamewataka wakulima kuzingatia usahuri wa wataalamu pindi wanaponunua mbegu,mbolea pamoja na madawa ya mazao.
Wakizungumza na Walter Habari baadhi ya wakulima wamesema kuwa wamekuwa wakiuziwa mbegu feki za kilimo hali inayowarudisha nyuma katika shughuli za kilimo na pia kuwasababishia njaa.
Martin Pius mratibu wa mviwata mkoa wa Manyara anasema mkutano wa mwaka huu umebeba kauli mbiu inayosema  Uhakika wa mbegu kwa uhakika wa chakula' lakini kauli mbiu hiyo anaeleza bado ni changamoto kwani Mbegu zinazosambazwa sio halisi.
Bwana Pius amewataka wasimamizi wa pembejeo za kilimo ikiwemo serikali iweze kufanya kazi yake kikamilifu ili kuweza kudhibiti tatizo hilo.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top