0
Mwenyekiti wake wilayani Arusha, Saitoti Zelothe
WAKATI majina ya wagombea wa nafasi mbalimbali ndani ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) yakiwa bado hayajawekwa hadharani, baadhi ya wanachama wa umoja huo wameibuka na kumtuhumu Mwenyekiti wake wilayani Arusha, Saitoti Zelothe kufanya kampeni wilayani Karatu.
Hata hivyo, Zelothe alipohojiwa kuhusu tuhuma hizo juzi alikanusha na kusema kwamba alikwenda wilayani Karatu kuhudhuria mazishi na tuhuma hizo zina lengo la kuchafuana kisiasa.
Alifafanua kwamba yeye ni kiongozi wa jumuiya hiyo ngazi ya wilaya, hivyo haoni tatizo kukutana na baadhi ya wanachama na watu wamekuwa wakitafisri kitendo cha kukutana na vijana hao kama kufanya kampeni.
Baadhi ya wanachama wa jumuiya ya umoja huo wamemlalamikia kiongozi huyo kwamba amekuwa akizunguka katika baadhi ya wilaya mbalimbali mkoani Arusha akiomba achaguliwe nafasi ya Mwenyekiti wa UVCCM mkoani Arusha na kwamba ana imani jina lake litarudi baada ya mchujo.
Lengai Ole Sabaya ambaye ni mwanachama wa umoja huo alisema kwamba kiongozi huyo amekuwa akizunguka na baaadhi ya makada wa umoja huo huku akiomba achaguliwe nafasi hiyo kwa madai kwamba ana uhakika jina lake litarejea.
Alisema kwamba mbali na kiongozi huyo kuonekana wilayani Karatu lakini pia ameonekana wilayani Meru hivi karibuni, akikutana na baadhi ya vijana wanachama wa jumuiya hiyo akiwaomba wachague jina lake pindi litakaporejeshwa. Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka alisema katika usimamizi wa haki na usawa ndani ya CCM, hakuna mtu anayebebwa na mtu.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top