Mzee
Joseph Sahn (60), mkazi wa Kijiji cha Nzonza wilayani Shinyanga amefia kwa
mganga wa kienyeji Robert Mkoma mkazi wa kijiji hicho wakati akimpatia matibabu
ya kumuongezea nguvu za kiume kwa kutumia pampu ya baiskeli.
Akizungumza
ofisini kwake leo Jumatatu, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Simon Haule
amesema tukio hilo lilitokea jana Jumapili saa 10:00 jioni nyumbani kwa mganga
huyo, alipokuwa anamuwekea dawa ya unga kupitia tundu la uume wake kisha kuanza
kuisukuma kwa kutumia pampu ya kujaza upepo kwenye baiskeli.
Kamanda
Haule amesema wakati akipampu ili dawa hiyo iingie vizuri ndani, mzee huyo alianza
kutokwa damu nyingi kwenye tundu hilo na kisha kuishiwa nguvu.
“Kutokana
na kutokwa damu nyingi ilisababisha kifo cha mzee huyo, ambapo tayari jeshi la
polisi linamshikilia mganga huyo kwa tuhuma za kusababisha kifo cha mzee
Joseph,” amesema Kamanda Haule
Amesema
mtuhumiwa atafikishwa mahakamani ili ajibu tuhuma zinazomkabili.
Kamanda
Haule aliwataka wananchi kuacha kuona waganga kuwa kimbilio la matatizo yao
badala yake wakimbile hospitalini au kwenye vituo vya afya vilivyokaribu nao.
Post a Comment
karibu kwa maoni