Ukosefu
wa waalimu maalumu kwa ajili ya kuwafundisha wanafunzi walemavu shuleni imetajwa kuwa ni changamoto kutokana na mahitaji ya wanafunzi
kuwa makubwa kuliko wanafunzi walioko.
Hayo yamebainika katika shule ya msingi Katesh A iliyopo mkoani
manyara wilayani Hanang’ inayofundisha wanafunzi walemavu na wale wasiowalemavu kwa kuwatengea madarasa maalumu pale wanapoanza kusoma kwa mara
ya kwanza na baadaye wakielewa madarasa ya awali ndipo huwachanganya
na wanafunzi wenzao wasio na ulemavu wa aina yeyote.
Shule ya msingi kateshi A ni shule pekee mkoani manyara yenye
kufundisha wanafunzi walemavu wa aina zote na wengine wakiwa wanakaa shuleni
huku wengine wakiwa ni wale wa kwenda na kurudi naa aina ya walemavu ni
walemavu wa akili,walemavu wa macho na viziwi lakini changamoto zimekuwa
ni nyingi kwa wanafunzi hao ikiwemo watoto wengi walemavu kufichwa majumbani na
wazazi wao.
Wakizungumza na wanafunzi hao shuleni hapo umoja wa wakuu
wakinamama shule za sekondari wilaya ya Hanang [UWAWASHUKA] walikuwa wakitoa msaada wa vitu mbalimbali vya kula walieleza kuwa wameguswa na kile wanachokifanya shuleni hapo na kuonekana kufanikiwa kwa
kiwango kikubwa kutokana na kupokea wanafunzi hao bila kujali aina ya ulemavu
walionao.
Bi.Esther Malongo ambaye ni mwalimu mkuu wa sekondari ya
Nagwa na Mwenyekiti wa chama hicho alieleza kuwa ni wakati wa
wazazi sasa kuwatoa watoto hao kutokuwafungia ndani na badala yake wawalete waje kuungna
na wenzao ili waweze kufuta ujinga kwani wanahaki ya kupata elimu ambayo
ndio mkombozi na mrithi wao kwa ajili ya kesho.
‘’Tumekuja kuwatembelea sisi kama wazazi wenu na kuwahamasisha ili mpate amani na msijione mko tofauti sana na wenzetu hapana wote mko sawa
na leo tumewaletea zawadi ili ziwasaidie lakini sisi kama wazazi wenu tunawapenda na tunataka msome mfike mbali ili muwe mfano wa
kuigwa kwa wenzenu ambao hawajaja shuleni lakini pia muwambie wazazi wenu
wasiwafungie ndani wawalete shuleni’’alisema Bi. Malongo.
Licha ya shule hiyo kuwa na wanafunzi walemavu lakini walemavu hao wanatajwa kuogoza katika masomo yao kila mwaka na wameongoza zaidi katika
miaka yote toka kuanzishwa kwa madarasa maalumu kwa ajili ya wanafunzi
walemavu mwaka 1996 na waliofeli kwa kipindi chote hicho ni wanafunzi
wanne toka kuanzishwa kwake.
Naye katibu wa chama hicho cha walimu wakuu wa kike wa sekondari Hanang’ ambaye pia ni mwalimu mkuu wa sekondari ya Masqaroda Bi.Gisela Msoffe alileza kuwa shule ni kiwanda kinachozalisha kupitia elimu na ili malighafi yako iweze kuuzika na kupendwa na wengi lazima iwe bora na huu ndio wakati wa wanafunzi hao kuweka mkazo kwenye elimu ili waweze kupata soko.
‘’Watoto tunawaomba muache kushaushika na makundi yaliyopo ambayo yanawapotosha
haswa yale ya utumiaji wa madawa ya kulevya hayo hayfai yatawaharibia maisha
yenu kwa haraka sana kuweni na nidhamu ili mzidi kuwa bora
zaidi’’Alisema Bi.Esther.
Neema Peter ni mwalimu wa wanafunzi wa walemavu wa akili shuleni hapo ambaye
anaeleza kuwa ukosefu wa walimu maalumu ili waweze
kutumia muda kidogo kwenye ufundishaji toofauti na ilivo kwa sasa ambapo hutumia
muda mwingi kufundisha kutokana na wanafunzi hao kutumia muda mwingi kwenye
kufanya kwa vitendo kuliko kusukiliza.
‘’Hatuzingatii muda maalumu uliotengwa na serikali kutokana na
uchache wetu walimu lakini pia hatupo wengi ni wachache sana hivyo tungeongezewa walimu wengine maalumu ili tuweze kusaidiana ingetusaidia sana’’alisema Bi. Neema.
Shule ya msingi Katesh A inakabiliwa pia na ukosefu wa vifaa vya
kufundishia wanafunzi hao hivyo unaiomba serikali kuwasaidia vifaa hivyo pamoja na wadau mbalimbali watakaoguswa kwa ajili ya kuwainua wanafunzi
hao ambao ili waweze kutimiza ndoto zao.
Post a Comment
karibu kwa maoni