Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na
rushwa nchini (TAKUKURU) Kamishna Valentino Mlowola amemtaka Mbunge wa
Arumeru Mashariki Joshua Nassari kutii sheria bila shuruti ya kukaa
kimya akisubiri taasisi hiyo kushughulikia taarifa alizopeleka za
kiuchunguzi kuhusu rushwa kutumika kuwafanya madiwani kuhama CHADEMA
kwenda CCM.
Mlowola amesema hayo jijini DSM wakati akizungumza na wanahabari na
kusisitiza kwamba endapo Nassari atakiuka agizo hilo na kuendelea kutoa
taarifa za mwenendo wa uchunguzi wa taarifa alizopeleka TAKUKURU
atafikishwa kwenye vyombo vya Sheria.
Post a Comment
karibu kwa maoni