0
Image may contain: 3 people, people standing, beard and indoorAliyekuwa mkuu wa wilaya ya Arumeru mkoani Arusha Alexander
Mnyeti amekaribishwa rasmi katika mkoa wa Manyara tayari kwa kuanza kutumiika
kama mkuu wa mkoa wa Manyara.
Mkuu wa mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti amesema viatu alivyopewa ni vikubwa lakini atajitahidi  kuvivaa kwa kushirikiana na wananchi wa Manyara na watumishi katika kuuletea mkoa Maendeleo.
Akizungumzia siasa Mnyeti amesema yeye kama  mkuu wa mkoa anasimamia ilani ya chama cha mapinduzi  na kutoa onyo  kwa wapinzani kwa wakati yeye yupo mkoani Manyara  kwamba wafiche makucha yao kwani hatkuwa tayari kusikia chama chake kinachafuliwa na yeyote.
Amesema yeye atafanya kama Mnyeti na hawezi kufanya kama Bendera,’Bendera alikuwa mpole sana ila mimi nitakuwa tofauti”.
Jimbo la Babati mjini linakaliwa na upinzani [CHADEMA] kuanzia madiwani na mbunge,katika kata nane CCM ilipata kata 3 pekee.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top