0


Mkuu wa wilaya ya Babati Raymond Mushi novemba 7, 2017 amezindua rasmi Umoja wa Walimu wastaafu wilaya ya Babati UWAWA wenye lengo la kusaidiana katika matatizo mbalimbali.
Lengo la kuanzishwa kwa umoja huo wa walimu wastaafu ni kusaidiana katika matatizo mbalimbali yanayowakabili walimu hao.
Mkuu wa wilaya Mushi amesema pamoaja na kuwa walimu hao wamestaafu lakini ndio chanzo cha kuleta Maendeleo na amani katika nchi na kufundisha maadili mema katika jamii.
Pia mushi amesema huu ndio wakati kwa walimu wastaafu kjiongeza katika kuleta mabadiliko katika maeneo yao kwa kutoa elimu mbalimbali kuhusu ujasiria mali,mabadiliko ya tabia nchi ili kukisaidia kizazi hiki katika kutunza mazingira yanayoharibiwa kwa shughuli za kibinadamu.
Na umoja huo unatarajiwa kusajiliwa kitaifa na kwa sasa wapo katika hatua za mwisho kukamilisha hilo.
Mkuu wa wilaya amewapongeza walimu hao kwa kuunga umoja huo huku akiahidi kushirikana nao bega kwa bega katika omoja huo.
Walimu hao wastaafu wameeleza kuwa wanajivunia kukutana pamoja na kushirikana kwani hilo linawapa faraja na furaha pamoja na kuwa na matumani.
Mzee Mosses Mbesere yeye ni mwalimu ambaye tangu astaafu ni miaka 25 sasa, alistaafu mwaka 1992 anasema mpaka sasa maisha yake yapo vizuri kwa sababu alijiwekea malengo kabla ya kustaafu huku akiwataka walimu wengine kutambua kuwa kuna maisha baada ya kustaafu hivyo waache mambo ambayo sio lazima katika maisha.
Mwalimu Mosses Mbessero aliestaafu miaka 25 iliyopita,na sasa anafanya shughuli za kilimo.
Umoja wa walimu wastaafu Babati UWAWA ulibuniwa mwaka 2016 na baadhi ya walimu wastaafu baada ya kuona hali ngumu ya  maisha ya walimu wastaafu pamoja na afya zao kuzorota hivyo ulisajiliwa chini ya vikundi na idara ya Maendeleo ya jamii, jinsia,watoto wazee na afya  6.2.2017 mpaka sasa una jumla ya wanachama 52 wakemo wanawake 18 na wanaume 34 huku wakiongozwa na katiba.
Wakati huo huo CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT) wilayani Simanjiro mkoani Manyara, kimewakabidhi walimu 10 wastaafu Sh milioni 3.4 kwa ajili ya ununuzi wa mabati 200.
Mwenyekiti wa CWT wilayani Simanjiro, Abraham Kisimbi aliyasema hayo wakati akizungumza kwenye mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika mji mdogo wa Orkesumet. Mwalimu Kisimbi wamewapa walimu hao wastaafu 10 fedha hizo kuwawezesha kupata jumla ya mabati 200 ambapo kila mmoja atapata mabati 20 yatakayowasaidia kuezeka nyumba zao watakazojenga na kuanza maisha yao ya ustaafu.
“Tumeona badala ya kuwapa mabati na kuhangaika kusafirisha kila mmoja tumempa hundi ya Sh 340,000 ili akanunue mabati 20 kule anapoishi,” alisema mwalimu Kisimbi. Aliwataka walimu hao kutumia fedha hizo kwa malengo yaliyopangwa ili wakafanikishe maisha yao kipindi hiki ambacho watakuwa wamestaafu kazi zao za ualimu na kuanza maisha mengine.
Mwalimu Nazama Tarimo akisoma risala ya CWT alisema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo walimu kutopandishwa madaraja, kutolipwa madai yao, kutembea umbali mrefu na msongamano wa wanafunzi madarasani kunasababisha walimu kushindwa kufikia asilimia 80 ya ufaulu kwa wanafunzi wa eneo hilo.
Mwalimu mstaafu Peter Toima ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali la ECLAT alisema kwa kutambua thamani ya elimu ameiunga mkono serikali kwa kukarabati, kukarafati na kujenga madarasa mapya kwenye shule mbalimbali.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top