0
Image result for railaKiongozi wa Muungano wa vyama vya upinzani nchini Kenya ambaye alikuwa mgombea urais wa nchi hiyo Raila Odinga na makamu wake Kalonzo Musyoka, wanatarajia kujiapisha leo kuwa Rais wa nchi hiyo.
Taarifa kutoka Kenya zinasema kwamba zoezi hilo linafanyika kwenye viwanja vya Uhuru Park jijini Nairobi, huku serikali ikiwaruhusu kutumia uwanja huo, na kuwataka askari polisi waondoke mitaani na kuwaacha huru wafuasi wa NASA.
Wafuasi wa NASA wameonekana wakifurika kwenye viwanja hivyo kutoka sehemu mbali mbali za nchi ya Kenya, lakini mpaka sasa viongozi hao wawili hakuna aliyejitokeza uwanjani hapo.
Taarifa zaidi zinasema waandishi waliokwenda nyumbani kwa kiongozi wao Raila Odinga wamezuiwa kuzungumza naye, baada ya wanafamilia kusema 'Baba' hayupo.
Kubwa zaidi ambalo limeibua hisia za Wakenya ni serikali kuzima baadhi ya vyombo vya habari vikiwemo televisheni na radio, kufuatia kurusha kwa matangazo ya kuapishwa Raila Odinga.
Ifahamike kwamba iwapo Raila Odinga na Kalozno Musyoka watafanikiwa kuapishwa, watakuwa wamefanya kosa la uhaini na jaribio la kupindua Rais aliyepo, kwani yupo kwa mujibu wa Katiba ya nchi ya Kenya na ameapishwa kisheria.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top