0

Image result for MWENYEKITI UVCCM TAIFA 
Chama cha mapinduzi  [Ccm] mkoa wa Manyara kinatarajia kuvuna wanachama zaidi ya mia tatu [300] kuelekea maazimisho ya miaka 41 ya chama hicho jumatatu Feb 5 kesho.
Hayo yamebainishwa na Katibu wa umoja wa wanawake wa Tanzania [UWT] Mkoa wa Manyara Haines Munisi wakati akizungumza na wanawake wa umoja huo katika kata ya Bonga na Babati mjini.
Bi Haines amesema kuwa katika kusheherekea miaka ya kuzaliwa chama hicho kila mwaka wanafanya shughuli mbalimbali ambapo kwa mwaka huu wanaazimisha kwa kukagua na kuweka miapaka kataika maeneo ya Chama,kupanda miti na kuwatembelea watu wenye mahitaji maalum wakiwemo wagonjwa waliolazwa Hospitalini,watoto yatima na kuwapatia misaada mbalimbali.
Image result for uwt manyara
Katibu wa umoja wa wanawake mkoa wa Manyara UWT Haines Munisi
Aidha amebainisha kuwa kwa mwaka huu UWT imejiwekea malengo ya kupata wanachama wapya ambapo mpaka kufikia Jumatatu Februari 5 mwaka huu wanatarajia kuwapokea wanachama zaidi ya mia mbili 200 kutoka vyama pinzani.
Mwenyekiti wa umoja wa vijana Ccm UVCCM Taifa Kheri James  akiwa mkoani Manyara ijumaa  Februari 2 .2018 katika kambi maalum ya vijana kata ya Kiru Babati vijijni  aliwakabidhi kadi wanachama wapya 130 waliokihama chama cha Demokrasia na Maendeleo [CHADEMA].
Kheri James  akizungumza na vijana hao aliwapongeza kwa kurejea Ccm na kuwahidi kuwa chama cha mapinduzi kimejipanga kuwaondolea vijana changamoto ya ajira inayowakabili

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top