0


Chama cha mapinduzi tarehe tano februari kinasheherekea miaka 41 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1977.
Katika kuelekea sherehe hizo  umoja wa wanawake Tanzania UWT mkoa wa Manyara wakiongozwa na Katibu wa umoja huo Haines Munis wamesema wanasheherekea miaka hiyo kwa kuwatembelea wagonjwa na kupanda miti ambapo leo wametembelea kituo cha Afya Bonga Halmashauri ya mji wa Babati na kutoa misaada mbalimbali kwa wagonjwa na wahudumu wa Kituo hicho ikiwemo sabuni.
Msaidizi wa Mganga mkuu mfawidhi  wa kituo cha afya Bonga Dk. Onesmo Ole Kimboria amesema zipo changamoto nyingi zinazokikabili kituo hicho ikiwemo kukosa usafiri wa kuhamisha mgonjwa aliyezidiwa,chumba cha X-Ray,chumba cha kuhifadhia maiti,uhaba wa vyumba vya kulaza wagonjwa.
Dk.Ole Kimboria ameomba halmashauri pamoja na baraza la madiwani kutatua changamoto hizo ili kuweza kutoa huduma bora za afya.
Pia Wakina mama kutoka UWT Manyara waliwatembelea wanafunzi kuwatembela watoto wenye mahitaji muhimu katika shule ya msingi Bonga na kuwapa msaada wa madaftari na kalamu.
Watoto hao ambao wameonekana wakiwa na huzuni muda mwingi huku wakitokwa na machozi kwa kile kinachoonekana kuwakumbuka wazazi wao waliowatoka duniani, wamewafanya wakina mama walofika kuwatembea nao kutokwa na machozi.
Hata hivyo watoto hao wameahidi kusoma kwa bidii na kuwasaidia wale wasiojiweza.
watoa machozi wakina mama hao waliofika darasani wakati wakifundishwa jumuiya tatu za chama hiko kinaendelea na shuguli mbalimbali za kijamii.
Kwa upande mwingine umoja wa wanawake wa Ccm Tanzania mkoani Manyara umeahidi kurudi tena shuleni hapo na kutoa misaada mbalimbali ikiwemo mavazi kwa watoto hao,vifaa vya shule na kuwapeleka baadhi yao katika shule zenye hosteli.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top