0


Image result for MASONGA CHADEMA
Chama  cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimekusudia kukata Rufaa kupinga hukumu iliyotolewa  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya dhidi ya washtakiwa ambao ni Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini Joseph Mbilinyi na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga.
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa ambaye pia alikuwa wakili upande wa utetezi Prof. Abdallah Safari amesema kuwa hawajaridhika na hukumu hiyo kwani hakuna sababu za msingi zilizopelekea washtakiwa hao kufungwa.
Prof. Safari amesema kuwa kwa sasa wamekwisha kukata rufaa na wanaomba dhamana ili wakati wa kusikiliza rufaa hiyo washtakiwa wawe nje ya kifungo.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top