0
Image result for wastara 
Muigizaji wa filamu nchini Tanzania, Wastara ameondoka nchini kuelekea India kwa ajili ya matibabu ya mguu wake ulioanza kumsumbua mwishoni mwa mwaka jana huku akiwashukuru watanazania na Vyombo vya Habari kwa kuwa pamoja naye kipindi alivyokuwa akihitaji msaada wa fedha.

Wastara akiongea na waandishi wa Habari jana Jumapili Februari 4, 2018 katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam, alisema “nina washukuru sana vyombo vya habari wote kwa moyo wa upendo walionesha kwa sababu bila ya wao hata mimi nisingekuwa Wastara. 

"Napenda kuwaambia watanzania kwamba tuamini sana maneno anayosema mtu kuliko neno analosema mtu mwingine kwa hiyo naamini kuna wengine watakuja na matatizo tujaribu kuwaangalia nawao pia”.

Na alipoulizwa kuhusu tuhuma za kutumia fedha za matibabu kwa starehe kama alivyowahi kuchangiwa kipindi cha nyuma na kwenda Dubai, Wastara alisema hajawahi kuchangiwa na Watanzania bali alisaidiwa na Makamu wa Rais na hakutumia kwa matumizi mengine.

“Kwanza niseme sijawahi kuchangiwa na Watanzania mimi kama mimi, mara ya kwanza nilipoumwa aliyenichangia asilimia kubwa alikuwa ni Makamu wa Rais, na uzuri ni kwamba mpaka nafika hospitalini nilikuwa nampigia simu. Kilichosababisha watu waseme baada ya kufika hospitali kama hivi ninavyokwambia wiki tatu linapotokea tatizo kama umefanyiwa Oparesheni au upasuaji wowote niliambiwa unauwezo wa kukaa au kuishi kwenye hoteli karibu na hospitali..Ndipo watu wa karibu yangu wa Oman wakawa wamenipa Visa nikaenda kukaa huko kwa muda.“alisema Wastara.
Ikumbukwe kuwa ni miaka mitano sasa tangu mume wake Sadick Juma Kilowoko maarufu kwa jina la Sajuki kufariki dunia baada ya  Kulazwa katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU), chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari, akisubiri kusafiri kwenda India kwa mara nyingine, kuendelea na matibabu
Alianguka jukwaani
Kabla ya kulazwaDesemba 18 mwaka jana, Sajuki alifikishwa hospitalini hapo akitokea jijini Arusha, baada ya kuanguka jukwaani kutokana na kuishiwa nguvu wakati alipopewa kipaza sauti kuwasalimia mashabiki waliofurika, ili kumtazama katika Tamasha la Asante Tanzania.
Tukio hilo lilitokea katika tamasha hilo lililohusisha wasanii wa filamu na wale wa muziki wa kizazi kipya lililofanyika  ndani ya Uwanja wa Sheikh Amri Abeid,  wakati msanii huyo alipopandishwa jukwaani kuwasalimia mashabiki wake.
Baada ya kupandishwa jukwaani, alipewa kipaza sauti ili aweze kuwasalimia mashabiki wake lakini katika hali ya kawaida alifanikiwa kutamka neno moja tu,”ahhh” na kisha kudondoka akiwa juu ya  jukwaa na kabla ya kutua chini, alidakwa na wasanii wenzake waliokuwa pembeni,”
Wasanii hao walimshusha jukwaani baada ya kumpumzisha kwa muda na kumtaka aende kupumzika zaidi. Akihojiwa baada ya tukio hilo, Sajuki alisema kwa sauti ya upole kwamba hali yake kiafya si nzuri kwa kuwa hana nguvu na anahitaji matibabu. ”Hali yangu si nzuri kabisa naumwa sana, sijisikii vizuri,”alisema Sajuki.
Haya ni maneno ya mwisho ya Sajuki kwa vyombo vya habari, wakati akiwa tayari amepitiliza siku zake za kurudi India, kuendelea na matibabu yake baada ya kukosa Sh28 milioni.
Wastara aliwahi kumwambia mwandishi wa habari hii kuwa,  Sajuki alipaswa kurejea India Desemba 6 mwaka jana, lakini alikwama kufanya hivyo kutokana na upungufu wa pesa. Hata hivyo  alisema  waliamua kuandaa matamasha mbalimbali kwa ajili ya kutunisha mfuko wa matibabu yake.
Tamasha la kwanza la wasanii hao lilifanyika mkoani Iringa Novemba 25 mwaka jana na kupambwa na wasanii wengi wa muziki na filamu. Tamasha lingine lilifanyika Desemba 18 jijini Arusha.
Ugonjwa wa Sajuki
Mwaka 2011 haukuwa mzuri kwa Sajuki kwani ndio mwaka ambao maradhi yaliyomsumbua kwa muda mrefu, yalipamba moto.
Sajuki aligunduliwa kuwa na ugonjwa wa uvimbe pembeni ya ini,  mapema mwaka 2011 alipoanza kuugua. Mei mwaka 2012 alifanikiwa kwenda India kwa matibabu na baadaye  alirejea nchini na kuonekana kuimarika kiafya, kabla ya kuanza kuugua tena.
Kwa mujibu wa Katibu wa Chama cha Waongoza Filamu wa Wilaya ya Ilala, Rajabu Amiri, hivi karibuni, Sajuki alikuwa anasumbuliwa na tatizo la upungufu wa damu,  uti wa mgongo na  kansa  ya ngozi.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top