0
Mwenyekiti wa Umoja wa vijana mkoa wa Manyara [UVCCM] Mosses Komba amewaambia wabunge wa upinzani kuwa kwa sasa watafute kazi nyingine za kufanya kwa kuwa watu wa kazi wamepatikana.

Ameyazungumza hayo alipokuwa akihojiwa na WALTER HABARI katika kambi yao maalumu ya kutoa mafunzo mbalimbali kwa vijana zaidi ya mia sita katika kata ya Kiru wilayani Babati mkoani Manyara.

Kambi hiyo iliyofungwa jana na Mwenyekiti wa umoja wa vijana Taifa [UVCCM] Kheri James na mkuu wa mkoa wa Manyara Alexender Mnyeti,Kheri alieleza kuwa kwa sasa kauli mbiu ya Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi ambaye ndiye Rais wa Tanzania John Magufuli NI KAZI TU ila kwa upande wa vijana kauli mbiu yao ni TUKUTANE KAZINI.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top