0
Image result for MAGUFULI
Leo Februari 5.2018 madiwani wa Halmashauri wa mji wa Babati Mkoani Manyara wamekutana na kujadiliana mambo mbalimbali ambapo pia suala la kituo kikuu cha mabasi Babati  kimetolewa ufafanuzi.

Katika ufafanuzi huo imeelezwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli ameikabidhi Stand ya Babati mjini Mkoani  Manyara kwa chama cha Mapinduzi [CCM].

Katika Barua iliyoandikwa kwa mkuu wa Mkoa Manyara Alexender Mnyeti na kusomwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Babati Fortunatus Fwema imeeleza kituo hicho cha Mabasi kinapewa Ccm badala ya Uwanja wa Mpira wa Kwaraa.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Babati [CHADEMA] Kibiki Mohamedi hakuridhishwa na hatua hiyo huku akisema kuwa suala hilo atalifikisha katika uongozi wa juu baada ya kushauriana na wazee katika kikao walichoketi Hotl ya White Rose mjini Babati mwishoni mwa mwezi wa kwanza mwaka huu.
Aidha amesema kuwa Busara waliotumia kuuachia uwanja wa Kwaraa kwa Matumizi ya Shule ya Msingi Babati na Osterbay anaamini pia itatumika katika suala ya kituo cha mabasi ambacho ndio kitega uchumi kikuu cha Halmashauri ya mji wa Babati.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top