0
Watanzania watatu na raia watano wa Nigeria wanashikiliwa na Idara ya Uhamiaji wakidaiwa kupatikana na dawa za kulevya zikiwamo Heroin, Cocaine, bangi na mashine ya kutengeneza dawa hizo. Kaimu Kamishna wa Usimamizi na Udhibiti wa Mipaka, Kagimbo Hoseah amesema watuhumiwa wamekamatiwa eneo la Masaki jijini Dar es Salaam.
Hoseah amewataja Watanzania kuwa ni Ruth Kabezi, Lucy Adolf na Lizzy Minja ambaye ni wakili wa kampuni ya Law Associates. Wanigeria wametajwa kuwa ni, Bisola Adeyemi, Olasunkanmi Kayode, Aaron Ejeh, Obina Nwauba na Darlington Nwauba.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top