0
Mbunge wa Nzega Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Hussein Bashe ameliandikia barua Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania ametoa hoja binafsi akitaka kuundwe Tume teule ya Bunge kuchunguza matukio yanayohatarisha Usalama wa Taifa.
Bashe ameyataja baadhi ya matukio ambayo angependa kamati hiyo iyachunguze ni pamoja na kusinyaa kwa demokrasia na haki za raia, kupotea, kutekwa, kuuawa kwa Raia na kupigwa risasi kwa raia na kikundi cha ‘watu wasiojulikana’.
 


Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top