0

Related imageBenki ya NMB Mkoani Manyara Tawi la Babati imetoa msaada wa Meza na Viti 47 kwa Chuo cha ualimu Mamire Kilichopo Wilayani Babati Mkoani humo. 

Akikabidhi Viti hivyo chuoni hapo vyenye thamani ya shilingi million 5 Meneja wa Benki hiyo kanda ya Kaskazini Stratton Chilongola alisema Masada huo ni kama sehemu ya ushiriki wao katika maendeleo ya Jamii. 

Alisema wamekuwa wakishiriki katika mambo mbali mbali ikiwemo kutoa vifaa vya shule kwenye shule zenye mahitaji pamoja kutoa misaada hospitalini na kwenye Maafa kama sehemu ya kurudisha fadhila kwa Wananchi ambao pia ni wateja wao.

Alisema wao kama benki wanahakikisha Kuwait wanasaidiana na serikali kutatua changamoto ambazo zinaikumba sekta ya Elimu na hivyo ili kufanikisha hilo benki ya NMB imetenga zaidi ya shilingi Billion 1 ili kusaidia jamii katika sekta za elimu na Afya kwa mwaka huu wa 2018.

 "Tunataka na sisi tuwe chachu ya maendeleo ya Watoto wetu, hawa walimu ndio watakao tufundishia watoto wetu tusiwaache wasome katika mazingira magumu, tuwatengenezee mazingira ambayo wataifurahia fani yao ya uwalimu" "Nawapongeza kwa juhudi zenu za kuhakikisha kuwatafuta wafadhili wa kuendelea kusaidia mambo mbali mbali katika chuo hiki ili kuhakikisha Walimu wetu watarajiwa wanatoka katika mazingira magumu '' alisema chilongola. 

Akipokea msaada huo Mkuu wa Wilaya ya Babati Raymond Mushi alisema Elimu ina manufaa kwa anayeipata na jamii nzima, hvyo kuwasaidia wanafunzi hao ili wasome katika mazingira bora ni njia moja wapo ya kuwatengenezea maisha bora wao na Taifa.

 "Nawapongeza Benki ya NMB pamoja na uongozi wa chuo kwa kutafuta wadau mbalimbali wa kuchangia Elimu, Serikali haiwezi kufanya kila kitu kwa wakati mmoja, hvyo kwa kushairikiana na wadau mbali mbali wa Elimu tunaweza kupiga hatua kubwa katika sekta hii ya Elimu "alisema Mushi.

 Aidha aliwataka Wanafunzi hao kuepukana na mambo mbali mbali ya ovyo ambayo yanaweza kuharibu Sifa zao na sifa za chuo hicho na badala yake kujikita katika masomo na kukumbuka kuwa wao ni walimu watarajiwa.


Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top