0



Kwa kawaida chama kilichopo madarakani ndicho ambacho kinakuwa na kauli kwani hata ilani inayotekelezwa huwa ni ya chama husika.
Hata viongozi wanaoteuliwa hufuata misingi na nyayo zilizopo ili kuleta msisimko wa Maendeleo katika Nyanja mbalimbali.
Mkuu wa mkoa wa Manyara Alexender Pastory Mnyeti amekuwa akitoa kauli ambazo zimekuwa zikiwakera wapinzani kwa namna moja ama nyingine.
Wakati akikaribishwa rasmi kuanza kazi katika mkoa wa Manyara alisema kuwa wapinzani waliopo katika mkoa huo watulie kwa kuwa ilani inayotekelezwa ni ya chama cha Mapinduzi.
Lakini pia hivi karibuni akiwa katika ziara zake za kikazi katika wilaya zake alisikika akisema
"Kwanza niwatambue CHADEMA kama nani? Mimi si NEC wala msajili wa Vyama vya Siasa.
Pili nishirikiane nao katika kutekeleza ilani ipi? Nimesoma ilani yote ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 sijaona mahali pametajwa CHADEMA, sasa nalazimika vipi kushirikiana nao?" ~ RC Mnyeti

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top