0
Polisi Mkoa wa Iringa wamemkabidhi Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi
Tanzania(TSNP), Abdul Nondo kwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya
Jinai, jijini Dar.

RC Makonda aliwataka Polisi Iringa kufanya hivyo baada ya kumaliza
kumuhoji kwa maelezo kuwa ameuchafua mkoa wa Dar es Salaam.

Makonda amesema Jeshi la Polisi limefanya kazi kubwa na hapendi kuona likichafuliwa na watu wachache.







Abdul Nondo alitoweka katika mazingira ya kutatanisha akiwa
jijini Dar es Salaam na baadae kuripotiwa kutekwa na watu wasiojulikana lakini
alikuja kupatikana mkoani Iringa ambapo imedaiwa alitupwa huko, jeshi la polisi
linaendelea kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo la kutekwa kwa kijana huyo.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top