0
Radar image of TiangongChombo cha anga za juu cha China kilichoharibika kimeingia katika anga la dunia asubuhi ya leo na kupasuka vipande vipande kikitarajiwa kuanguka Kusini mwa Bahari ya Pasifiki. Kituo cha anga za juu cha China kimesema kupitia mtandao wake, kwamba chombo hicho, Tiangong-1, kimeingia katika anga la dunia saa 2 na dakika 15 saa ya China, na kusisitiza kuwa hakitasababisha uharibufu wowote. Awali, wataalamu wa masuala ya anga za juu walikuwa wamesema ingekuwa vigumu kujua chombo hicho kingeanguka sehemu gani, hadi muda mfupi kabla ya kuingia katika anga la dunia. Chombo cha Tiangong-1 kilipelekwa anga za juu mwaka 2011, ikiwa hatua kubwa kwa China katika juhudi za kujenga kituo chake binafsi cha anga za juu. Mwaka 2016 chombo hicho kiliharibika, na wanaanga wamekuwa wakisubiri kurejea kwake duniani. China imekanusha taarifa za vituo vya anga vya kigeni, kwamba imepoteza udhibiti wa chombo hicho.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top