0
Kampuni ya Orion Span ya Marekani imetangaza kujenga hoteli ya kwanza ya angani. Hoteli hiyo itafunguliwa mwaka 2022 na gharama ya kukaa katika hoteli hii kwa siku 12 ni dola za kimarekani Milioni 9.5.
Kampuni hiyo imesema inapanga kurusha hoteli ya angani iitwayo “stesheni ya Aurora” mwaka 2021. Hoteli hiyo itakuwa na vyumba ambavyo kila kimoja kina urefu wa mita 13 na upana wa mita 4, ukubwa wa vyumba vya hoteli utakuwa karibu sawa na ukubwa wa ndege aina ya Gulfstream G550.
Mpango huo bado uko kwenye kipindi cha kukusanya uwekezaji, lakini sasa watu wanaweza kuweka nafasi safari ya kwenda hoteli hiyo kwa kulipa dola za kimarekani elfu 80 kama amana ya kwanza.
Habari zinasema kwenye hoteli hiyo watalii watapata kuishi kama wanaanga, kuhisi ukosefu wa nguvu za mvutano wa dunia, kupiga picha ya dunia, kufanya majaribio ya kisayansi, kupanda mboga, kutazama mwanga aina ya aurora. Lakini kabla ya kwenda watalii wanahitaji kupata mafunzo kwa miezi mitatu.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top