
Kwa mujibu wa Mbunge huyo, huo unaotumika bungeni una makosa matatu yakiwemo ya maneno, ala na midundo.
Ameyasema hayo kwenye kikao cha kwanza cha Mkutano wa 11 wa Bunge wakati anaomba mwongozo wa Spika baada ya kipindi cha maswali na majibu.
Kwa mujibu wa Mapunda, wimbo wa taifa unaotumika bungeni ni tofauti na ulioidhinishwa na lililokuwa Baraza la Muziki Tanzania (BAMUTA) na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA).
Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson amesema, kabla ya kutoa mwongozo ni lazima ajiridhishe kwa kuusikiliza kwanza.
“Kwa hiyo kama kutakuwa na makosa nitatoa mwongozo hapo baadaye” amesema Dk. Ackson.
Post a Comment
karibu kwa maoni