0
Image result for MOFUGA MBULU 
Mkuu wa wilaya Mbulu Chelestino Mofuga ameligiza jeshi la polisi wilaya ya Mbulu kuwakamata watu wanaopaki magari katika uwanja wa Mbulu mjini kwani wanaharibu uwanja huo.
Akiongea wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi wa bonanza la pasaka lililofanyika katika uwanja wa mbulu mjini alisema kunatabia ambayo imezuka ya watu kutoeshimu uwanja huo kwani wanapaki magari yao wakati kuna sehemu nyingi ya kupaki na wengine pia wakijisaidia kwenye huo uwanja huku wakiwa wanajua kabisa inatumiwa kwa michezo mbali mbali na sherehe jambo ambalo siyo la kiungwana.
"Nina waagiza jeshi la polisi mkiona mtu amepaki gari lake kwenye uwanja huu chukua gari lake kalipumzishe pale kituoni watuchangie halmshauri ya mji kodi"
"Naomba kabisa na mnisikie kwa makini tuwe wastaarabu kila mmoja huu uwanja anahuitaji na wale wengine watakaopatikana wanajisaidia hapa hatua kali dhidi yao zitachukuliwa na nazani watakuwa mfano" alisema Mofuga.
Alisema na wale wote wanaokatiza kati katika uwanja huo wakati mazoezi au mechi ikiwa inaendelea nao waache mara moja kwani uwanja ni kwa ajili ya michezo na si njia ya wapita kwa miguu hivyo atakae onekana akipita kati kati nae akamatwe na polisi.
Katika bonanza hilo la pasaka lililoshirikisha jumla ya timu 8 kutoka wilaya ya Mbulu bingwa alikuwa ni Matipa fc baada ya kuwachapa Sinde fc mabao 3-2 kwenye mchezo wa fainali.
Mshindi wa kwanza ambae ni Matipa fc alipata zawadi ya Mbuzi mnyama mwenye thamni ya  shilingi 50,000,mshindi wa pili Sinde fc akapata 20,000

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top