0
Barabara ya kuelekea Airport Dodoma MjiniSERIKALI imesitisha uendelezaji wa maeneo ya Mji wa Serikali na Chamwino na eneo linalozunguka maeneo hayo mkoani Dodoma.
Katika maeneo hayo yaliyositishwa ujenzi kuna vijiji vya Msanga, Chahwa, Vikonje, Buigiri, Chamwino, Mahomanyika na Kikombo, kutokana na kufanyika ujenzi holela na mauziano ya ardhi yasiyo rasmi unaoendelea. Katika Tangazo lililotolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi linasema kutokana na ufanyaji mapitio ya mpango kabambe wa Mji Mkuu wa Dodoma unaoendelea kuna umuhimu wa kusitisha shughuli za uendelezaji ardhi katika maeneo hayo.
Pia maeneo yaliyo katika Tangazo la Serikali Namba 912 la Juni 30, mwaka jana ili kupisha au ukamilishaji wa suala hilo. Alisema katika kutekeleza uhamishaji wa Mji Mkuu wa Serikali kutoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma, serikali inafanya mpango kabambe wa Dodoma (2010), ili kuendana na mahitaji halisi ya uhamasishaji makao makuu una fursa nyingine za kiuchumi pamoja na mapitio ya mpango huo.
Serikali imeandaa mpango wa eneo la mji wa Serikali katika eneo la Ihumwa. Alisema kuzingatia Kifungu cha 8 cha Sheria ya Ardhi Sura 113 na Kifungu cha 5 kikisomwa sambamba na Kifungu cha 75 (a-c) cha Sheria ya Mipango miji, Sura 355 “nazielekeza Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma na Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino ambazo ndiyo Mamlaka za upangaji kusimamisha ujenzi holela na mauziano yasiyo rasmi ili kusubiri kukamilika kwa upangaji wa Mji wa Dodoma”.
CHANZO: HABARI LEO.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top