0
Upande
wa mashtaka wa kesi inayowakabili viongozi saba wa Chadema, akiwemo
Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe ameiomba Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu iruhusu kesi hiyo isikilizwe kwa haraka, ikiwezekana jambo
hilo kuanza kesho.

Wakili huyo wa Serikali, Faraja Nchimbi  amesema msingi wa  maombi hayo ni kutokana nai upelelezi kukamilika.

Amesema
sababu nyingine ni kwamba washtakiwa wengi katika kesi hiyo ni wabunge
na kwa kuwa kesi hiyo inavuta watu wengi ni vema ikasikilizwa haraka.

"Kwa
hiyo tunaomba kama ikiwezekana kesho mchana tuendelee na usikilizaji wa
awali ili sisi upande wa mashtaka tuweze kuwasilisha kile tulicho
nacho,” amesema Nchimbi.

Hata
hivyo, wakili wa upande wa utetezi,  Peter Kibatala amepinga
mapendekezo hayo akieleza kuwa ndiyo kiongozi wa jopo la mawakili wa
utetezi, kesho atakuwa na kesi nyingine Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi
na kesho kutwa pia atakuwa na kesi nyingine.

Amesema
Aprili watakuwa na semina za mawakili ambazo ni za lazima kwa kuwa bila
kupata alama zinazohitajika kutokana na semina hizo, leseni yake
haiwezi kuhuishwa.

Vilevile,
amesema kuanzia Aprili 13 watakuwa na mkutano wa mawakili wote jijini 
Arusha na akapendekeza usikilizwaji wa awali  wa kesi hiyo ufanyike
Aprili 16.

Katika
uamuzi wake, Hakimu Wilbard Mashauri amekubaliana na mapendekezo ya
upande wa utetezi na akaamuru usikilizwaji wa awali ufanyike April 16,
2018.

Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi tarehe hiyo, itakapoitwa kwa ajili ya usikilizwaji wa awali.

Mbali
ya Mbowe viongozi wengine walioachiwa kwa dhamana ni Katibu Mkuu Dk 
Vicent Mashinji, Manaibu Katibu Wakuu John Mnyika (Bara), Salum Mwalimu
(Zanzibar), Mbunge wa Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa,  Mweka Hazina
wa Baraza la Wanawake wa chama hicho Ester Matiku  na mwenyekiti wa
baraza hilo, Halima Mdee.
Nje ya Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu Dar es Salaam Mara baada ya kuachiwa Mwenyekiti
wa (CHADEMA) Mhe. Freeman Mbowe amefunguka na kusema
kuwa walipokuwa magerezani wameshuhudia mengi na watayaweka wazi
karibuni.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top