0
Leo May 10, 2018 Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga wameachiwa huru kutoka Gereza Kuu la Ruanda mkoani Mbeya ambapo walikuwa wanatumikia kifungo cha miezi 5.
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe amethibitisha kuachiwa kwa Viongozi hao wawili na tayari Sugu ameshafika nyumbani kwake.
Wengine waliofika gerezani kumpokea ni Meya wa Jiji la Mbeya, Mchungaji David Mwashilindi na madiwani, Mbunge wa Viti Maalumu, Sophia Mwakagenda

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top