Kampuni ya DSTV Tanzania imemdhamini
mshindi wa tano mtanzania Alphonce Felix Singu kutoka Singida mashindano ya
riadha Olympic mbio ndefu yaliyomalizika mwaka huu miezi michache iliyopita huko Rio
de Janeiro nchini Brazil kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Singu ameushukuru uongozi wa DSTV
kwa kumsimamia huku akiwataka wengine wajitokeze kusaidia wana riadha amabao
wapo wengi hawana wafadhili.
Mwanariadha huyo ameeleza kuwa mbinu
anazotumia katika riadha na kupata ushindi ni mazoezi ya mara kwa mara bila
kukata tamaa akiwapa moyo wanaraiadha wenzake kujituma biloa kuchoka kwani
mafanikio katika riadha ni makubwa.
'Sisi watu wa riadha kupata msaada
ni ngumu kidogo cha kufanya ni sisi kujituma,ukishafanya jitihada watu watakuja
wenyewe watakufuata"alisema Singu.
Alex Singu mshindi namba tano. |
DSTV wanaorusha michezo mbali mbali
ya kimataifa ikiwemo ile maarufu ya ligi kuu soka ya UINGEREZA EPL wameamua
kumsimamia Singu kwa kipindi cha mwaka mmoja ili kuzidi kutoa motisha na kuwapa
moyo washiriki wengine wa Mashindano kama hayo.
Sambamba na hilo Meneja wa DSTV
Tanzania Salum Salum amemzawadia King'amuzi cha DSTV bingwa wa riadha Tanzania
anaetokea mkoani Manyara Ismail Juma katika mshindano mbalimbali,mashindano ya
taifa 2016 katika mita 5000,mita 10000,Kilimanjaro half Marathon mshindi namba
moja,CROSS COUNTRY iliyofanyika nchini CHINA mwaka 2015 alishika namba tisa [9]
na kuipeperusha bendera ya Tanzania.
Salum amemkabidhi Kingamuzi hicho
pamoja na Dish lake ili aendelee kufuatila michezo mbali mbali duniani huku
wakimtaka aongeze juhudi zaidi..
"Kupitia riadha nimejenga na
ninaisaidia familia yangu lakini pia imenisaidia kuzijua nchi mbalimbali
duniani na kupata heshima'alisema Ismail Juma
Ismail ameshiriki mashindano makubwa
nchini Brazil alikuwa wa kwanza mwaka 2012 Kilomita 10 na kilomita 21, miezi
mitatu aliishi Brazil, China 2015,Nigeraia 2016 alishika nafasi nya pili
Kilomita 10.
Ismail anasema ugumu anaokutana nao
katika mazoezi ni kukosa lishe na matunda ambayo ni muhimu kwa afya.
Meneja Wa DSTV amesema kuwa kuona ni
kuamini hivyo wameamua kumleta Singu kama balozi Manyara kwa kuwa ndipo chimbuko la wanariadha wengi
ili kuwapa moyo ziadi wengine na kueleza kuwa wamevutiwa na kiwango cha Ismail
Juma.
Meneja wa Kampuni ya DSTV Tanzania,Salum Salum |
Naye Singu amekubali kiwango cha
Ismail na kukiri kuwa alishiriki nae mwaka jana katika mashindano ya riadha
yanayojulikana kama Cross Country yaliyofanyika nchini China yeye akishika
nafasi ya 49 huku Ismail akishika nafasi ya 9.
Post a Comment
karibu kwa maoni