Polisi
wilayani Geita mkoani Geita wametakiwa
kuchunguza kifo cha kijana Chacha Gairige aliyeuawa kwenye mgodi wa Geita
GGM tarehe 20 septemba majira ya saa
11:30 na kuwakamata walinzi wa mgodi huo wa dhahabu wanaotuhumiwa kufanya
mauaji hayo.
Chacha ni
mkazi wa Geita na alikuwa mchimbaji mdogo wa madini ya dhahabu katika mgodi
huo.
Kisa cha
kuuawa kwake kinasemekana kuwa ni pale alipoingia katika machimbo hayo kuchukua
mabaki ya madini [magwangala].I
Mkuu wa
wilaya ya Geita Herman Kapufi ametaka uchunguzi ufanyike haraka na wahusika wachukuliwe hatua
za kisheria.
Kwa mujibu
wa rafiki yake Nelson Busumagu [18] mkazi wa Msufini mjini Geita ambaye
walikuwa pamoja siku hiyo anaeleza kuwa
walinzi hao walimpiga jiwe kichwani kisha kumtumbukiza kwenye shimo lenye kina
kirefu chenye maji na mwili wake
kuonekana ukielea ndani siku ya pili.
Chacha
aliuawa kikatili huku Nelson akijeruhiwa sehemu mablimbali za mwili wake.
Kamanda wa
polisi mkoani Geita Mponjoli Mwabulambo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na
kueleza kuwa waliuopoa mwili wa Chacha baada ya kuonekana ukiwa unaelea katika
shimo lenye maji katika mgodi huo.
Post a Comment
karibu kwa maoni