WatuWatatu Wamehukumiwa Kifungo cha Maisha Jera Mkoani Kagera Baada ya kukutwa na hatia ya Kuchoma Makanisa Mkoani humo.
Hukumu hiyo imetolewa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa
Mahakama ya Mjini Bukoba na Hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo
Namba 178 na Namba 67 Victor Bigambo amewakuta na hatia baada ya
kusikiliza pande zote husika na kujiridhisha na ushahidi uliotolewa
Mahakamani hapo.
Akizungumza na Waandishi wa habari Nje ya Mahakama hiyo
Mjini Bukoba Naendesha Mashitaka Mayele Emmanuelly amesema kuwa
washitakiwa hao katika kesi Namba 178 pamoja na 67 wamehukumiwa Maisha
huku katika shauri la kula njama katika kesi hiyo Namba 67 wamehukumiwa
Miaka Saba.
Amewataja washitakiwa hao kuwa ni pamoja na Ngesele Joseph,
Rashid Mzee na Mwingine aliyetambuliwa kwa Majina ya Aguli Dauda ,
amesema kuwa Nje na mashauri hayo wawili lakini pia kuna mashauri zaidi
ya 16 ya uchomaji wa Makanisa Mkoani humo na pamoja na mengine kati ya
hayo ya Mauwaji.
Nae Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Kagera Augustine
Olomi amesema kuwa Wananchi waendelee kutoka TAARIFA kwa Kesho hilo ili
kuwabaini watu wengine waliohusika na Vitendo hivo na kwamba wao kama
Walinzi wa amani watahakikisaha Wananchi Wanalindwa na Mali zao.
Post a Comment
karibu kwa maoni