Aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Edward Lowassa amesema kuwa michango bado
inahitajika kwa wahanga wa Tetemeko LA ardhi Mkoani Kagera.
Bw:Lowassa amemueleza hayo Mkuu wa
Mkoa wa Kagera baada ya kuwa ametembelea katika Kara za Hamugembe pamoja na
Kashai Manispaa ya Bukoba na kujionea Namba watu na Majengo walivyo athirika
kutokana na tetemeko LA ardhi lililotokea septemba 10 Mwaka huu.
Amesema kuwa baada ya kujionea
madhara hayo ambapo makazi ya Wananchi hao yameathiriwa vibaya amechangia
Mifuko Mianne (400) ya Simenti huku akimuomba Mkuu wa Mkoa huo wa Kagera
Kutafuta wataalamu wa Video kutengeneza Makala zitakazo rushwa ili kuwa wezesha
Wadau Mbalimbali wa Maendeleo kujionea hali ambayo tetemeko hilo lilivokuwa
hususan kwa wale ambayo hawakufanikiwa kufika Mkoani Kagera.
Hata hvyo amesema kuwa Mchango wake
huo wa mifuko hyo 400 Inakadiliwa kuwa na thamani ya Shilingi Milioni Saba(7)
ambayo amesema kuwa itakabidhiwa kwa Meya wa Manispaa hiyo ya Bukoba.
Post a Comment
karibu kwa maoni