Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Magufuli
amesema kuwa huu ni wakati mwafaka kwa muswada wa sheria ya huduma za
vyombo vya habari kukubaliwa na kuwa sheria kwa vile tasnia ya habari
inakumbwa na changamoto nyingi zitakazotatuliwa na sheria hiyo.
Rais Magufuli akiongea na waandishi wa Habari Ikulu Magogoni jijini Dar es Salaam. |
Akizungumza
na wahariri pamoja na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari jana,
Ikulu jijini Dar es Salaam Rais Magufuli alisema kuwa muswada huo ni wa
muda mrefu na sasa ni wakati mwafaka kwa vile tansia ya habari inakumbwa
na changamoto nyingi zinazoweza kutatuliwa na muswada huo.
“Hii
sheria ya huduma za vyombo vya habari imechelewa kwa vile mchakato wake
ulianza tangu mwaka 2011 hadi sasa mwaka 2016 wadau walikuwa na muda wa
kutosha wa kujiandaa na kutoa maoni yao ambayo yangeweza kuboresha
muswada huo” alisema Rais Magufuli
Ameongeza
kuwa, Sheria hii italeta mabadiliko katika tasnia ya habari kwa vile
kutakuwepo na Bodi ambayo itashughulikia masuala ya taaluma ya habari,
pamoja na mambo mengine yaliyoanishwa katika muswada huo ambayo ni
maslahi ya waandishi wa habari nchini.
Muswada
huu unatazamiwa kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili waweze
kufanyakazi kitaalamu kwa kuandika na kutangaza habari zenye ukweli
zitakazochangia katika harakati za kuleta maendeleo kwa nia ya
kuwasaidia watanzania na serikali kwa ujumla katika kufikia malengo
yake.
Muswada
wa Sheria ya huduma za habari umesomwa jana Novemba 4, 2016 katika
kikao cha tano cha Bunge na mkutano wa 11, ambapo utajadiliwa na kufuata
taratibu zingine kabla ya kuwa sheria.
Post a Comment
karibu kwa maoni