Imeelezwa kuwa ukosefu wa mabweni
katika shule za Sekondari zilizopo maeneo ya vijijini ni moja ya vyanzo
vinavyochangia Wanafunzi wa kike kushindwa kuendelea na masomo, hali
inayopelekea kufifisha ndoto zao.
Hayo yamebainishwa na baadhi ya
Wadau wa elimu na wanafunzi wa shule ya sekondari ya GENDA wilayani MBULU
mkoani MANYARA wakati wa Harambee ya kuchangia ujenzi wa Bweni la Wasichana wa
shule hiyo, ambapo zaidi ya shilingi milioni 45 zimepatikana kutoka kwa wadau
mbalimbali.
Mbunge wa Jimbo la HANANG, MARY NAGU
amesema njia pekee ya kuondokana na umaskini, jamii inapaswa kubadili mtazamo
kwa kuhakikisha mtoto wa kike anapata elimu bora ili kuwa na jamii ya watu
wenye uwezo wa kumudu mazingira yao na kuleta maendeleo.
Post a Comment
karibu kwa maoni