Wabunge wa
bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wametakiwa kutopitisha makubaliano ya
kiuchumi kati ya Afrika mashariki jumuiya ulaya [EPA] muswada unaotarajiwa
kupelekwa bungeni na kujadiliwa alhamisi ya wiki hii.
Hayo
yamesemwa na mratibu wa mviwata Mkoa wa Manyara Martin Pius wakati akizungumza na manyara fm leo katika
mkutano wao mkuu wa tisa wa mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania Mviwata
uliofanyika Babati na kuzikutanisha wilaya zote tano za manyara zenye wanachama
wa mviwata.
Mratibu huyo
ameeleza kuwa endapo wabunge watakubali kupitisha makubaliano hayo ya uchumi
Tanzania na jumuiya hiyo ya Ulaya [EPA]yatawabana na kuwaumiza wakulima kwa kuwa masharti yake ni magumu.
Hata hivyo
mkataba huo unakwenda kujadiliwa huku tayari ikiwa wabunge wameshapatiwa semina
kuhusu mkataba huo wasomi na wataalamu
wakitahadharisha Tanzania iangalie faida na hasara kabla ya kuingia kwenye
mkataba ambao huenda ukaligharimu Taifa.
Nchi za Afrika mashariki zilizojiunga na EPA ni pamoja na nchi jirani ya Kenya.
Post a Comment
karibu kwa maoni