Kamanda Muliro akionesha dawa za kulevya zilizokamatwa na jeshi hilo -Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Jeshi
la polisi mkoa wa Shinyanga limemfukuza kazi askari wake mwenye namba
F9899 PC Hassan Mavindi kwa fedheha kutokana kujihusisha na dawa za
kulevya kwa makosa ya kukosa uadilifu wakati wa vita dhidi ya dawa za
kulevya.
Akitoa
taarifa kwa vyombo vya habari leo Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga
ACP Muliro Jumanne Muliro amesema jeshi hilo linahitaji vita hiyo
ifanyike kwa kiwango kikubwa cha uadilifu na umakini mkubwa unaotakiwa
kwa askari wakati wa ufuatiliaji wa taarifa.
“Kwa
maskitiko makubwa kuanzia Februari 12,2017 jeshi la polisi limeamua
kumfukuza kazi askari namba F 9899 PC Hassan kwa fedheha baada ya mfumo
wote wa kisheria kuuzingatia,mfumo wa haki”,amesema Muliro.
“Askari
huyu alifanyiwa mashtaka ya kijeshi na ushahidi wa kutosha dhidi yake
ukatolewa ikabainika hana uadilifu katika zoezi hili ambalo sisi tunaona
ni vita kubwa”,ameeleza Muliro.
Amesema
jeshi hilo litamfikisha mahakamani askari huyo na kwamba halitavumilia
askari yeyote atakayebainika kujihusisha na kutumia dawa za kulevya.
Hata
hivyo kamanda Muliro hakuweka wazi kama askari huyo alikamatwa
akisafirisha,akiuza au kutumia dawa za kulevya ambapo alisisitiza kuwa
wamemfukuza kazi kwa kujihusisha na dawa za kulevya kwa fedheha kwa
makosa ya kukosa uadilifu wakati wa vita dhidi ya dawa za kulevya.
Kamanda Muliro amesema pia watu wengine 33 wamekamatwa kwa kusafirisha,kuuza na kutumia dawa za kulevya.
Amesema
watuhumiwa hao 33 wamekamatwa wakati wa operesheni kali ya kuzuia na
kupambana na dawa za kulevya ya wiki mbili iliyoanza Januari 30,2017
ambayo wiki ya kwanza walijikita katika kuzifuatilia kwa siri za umakini
wa hali ya juu taarifa zote za kiintelijensia zinazohusiana na dawa za
kulevya.
Amesema
baada ya kuzichuja vizuri taarifa hizo kwa lengo la kuepuka
ubambikizaji wa kesi walifanya operesheni kwa vitendo kwa upekuzi na
ukamataji wa watuhumiwa kuanzia Februari 6,2017.
“Tulikamata
gramu 480 za heroine na cocaine,bangi kilo 81,kete za bangi
1,370,misokoto 1,230 ya bangi,mirungi kilo 3 na gramu 1,027 pamoja na
vifaa saidizi vya kujidungia dawa za kulevya ikiwemo sindano na bomba za
sindano 8 zenye ujazo wa CC 0.5”,ameeleza Muliro.
Post a Comment
karibu kwa maoni