Vita
dhidi ya Dawa za Kulevya sasa imeshika kasi, mara baada ya Kamishna
Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya Dkt. Rogers
William Sianga kutangaza kuanza na majaji na mahakimu waliovurunda
kwenye kesi zinazohusu dawa za kulevya
Sianga
aliyeapishwa jana na Rais Magufuli, ametoa tamko hilo leo wakati
kupokea kijiti kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Poul Makonda
ikiwa ni pamoja na kukabishiwa majina ya watu 97 ya wafanyabiashara
wakubwa, wanaotuhumiwa kujihusisha na dawa za kulevya.
Kamishna
Sianga amesema kuna mahakimu na majaji ambao wamekuwa wakivuruga kesi
za watuhumiwa wa dawa za kulevya ambapo pia amesema watapitia kesi zote
za madawa ya kulevya ili kuwabaini na kisha watapeleka orodha kamili
katika mamlaka husika ili hatua zichukuliwe.
Akitolea
mfano wa kesi ambazo amedaia zilivurugwa na mahakimu, amesema kuna kesi
moja ambapo ushahidi ulikuwa wazi kuwa mtuhumiwa amemeza dawa za
kulevya, lakini hakimu akasema kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa na matatizo
ya vidonda vya tumbo.
Pia
Sianga ameagiza kukamatwa kwa maafisa wa polisi waliosaidia kuingiza
viwatilifu vya kutengeneza dawa za kulevya nchini kiasi cha takriban
tani 21.
Naye
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe Poul Makonda amesema katika mkoa huo
kuna bandari bubu 54 huku 27 zikiwa zinatumika kupitishia dawa za
kulevya.
Pia
amesema kuna takriban nyumba 200, hoteli 67, Club 20 na vijiwe 107
vinavyotumika kusambaza na kuuza dawa za kulevya huku akibainish kuwa
kwa utafiti alioufanya, kila siku katika jiji hilo, kati ya kilo 10 hadi
15 husambazwa na kumalizika kila siku.
Mkutano
huo wa mapambano ya dawa za kulevya uliofanyika kwenye ukumbi wa Kituo
cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam
ulihudhuriwa pia na viongozi wa kidini, wanasiasa, wabunge, madiwani,
wakuu wa idara mbalimbali katika halmashauri za mkoa wa Dar es Salaam,
wadau mbalimbali wa mapambano ya dawa za kulevya pamoja na waathirika
wadawa za kulevya.
Post a Comment
karibu kwa maoni