
VODACOM na TIGO kuunza kuuza hisa soko la DSE
Hisa
za kampuni za simu za Vodacom na TIGO zitaanza kuuzwa katika soko la
hisa la DSM- DSE- mwishoni mwa mwezi Januari 2017 ili kuongeza ushiriki
wa watanzania kwenye umiliki wa kampuni hizo.
Uuzaji wa hisa, DSE.
Hisa za kampuni za simu za Vodacom na TIGO zitaanza kuuzwa
katika soko la hisa la DSM- DSE- mwishoni mwa mwezi Januari 2017 ili
kuongeza ushiriki wa watanzania kwenye umiliki wa kampuni hizo.Afisa mwandamizi wa DSE MARY KINABU amesema hisa za k ampuni hizo zitaorodheshwa katika Soko la Hisa la DSM baada ya kuuzwa katika soko la awali IPO.
Kuhusu mauzo ya hisa katika soko la hisa la wiki iliyopita KINABO amesema mauzo yamepanda na kufikia shilingi bilioni 5.3 kutoka shilingi bilioni 1.2 za wiki iliyotangulia.
Post a Comment
karibu kwa maoni