Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mkuu wa Mkoa wa Manyara Dkt Joel Bendera alisema kuwa ziara hiyo inatarajiwa kuanza rasmi tarehe 15 februari hadi tarehe 20 mwaka 2017 ambapo pamoja na mambo mengine atashuhudia sala maalumu ya kuombea amani katika maridhiano ya kuhitimisha uhasama uliokuwepo kati ya wakulima na wafugaji Wilayani Kiteto.
Alisema Waziri Mkuu akiambatana na Viongozi mbalimbali wa kitaifa atawasili tarehe 15 februari saa tatu asubuhi Wilayani Kiteto ambapo atalakiwa na viongozi mbalimbali wachama na Serikali wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Katibu Tawala pamoja Kamati za Ulinzi na usalama za Wilaya na Mkoa .
Pia akiwa Wilayani Kiteto ataweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa ofisi za Halmashauri ya Wilaya hiyo na kuongea na wananchi kwenye mkutano wa hadhara utakaofanyika katika uwanja wa michezo uliopo mjini kibaya.
Dkt Bendera alifafanua kuwa tarehe 16 februari Waziri Mkuu atafanya ziara Wilayani Simanjiro ambapo natapokea taarifa ya Wilaya na kuzungumza na watumishi wa umma katika ukumbi wa Halmashauri hiyo ambapo pia atasalimiana na wananchi wa Mji wa Orkesumrt na kukagua mradi wa upimaji wa viwanja na kuona mradi wa barabara ya KIA –Mirerani .
Tarehe 17 februari alisema kuwa Waziri Mkuu atakuwa Wilayani Mbulu ambapo atatembelea Hospitali ya Rufaa ya Haydom ambapo atapokea taarifa fupi ya hospitali hiyo na kuongea na watumishi wa Umma wa Wilaya ya mbulu, wananchi wa mji wa mbulu katika uwanja wa Getini.
Tarehe 18 februari Waziri Mkuu atakuwa Wilayani Hanang’ ambapo atapokea taarifa ya Wilaya na kuzungumza na watumishi wa umma na kuzindua majengo ya madarasa ya shule ya msingi Mogitu na ataongea na wanachi wa Mji wa Kateshi kupitia mkutano wa Hadhara katika uwanja wa shule ya msingi Kateshi.
Aidha akiwa Wilyani Babati tarehe 19 atapokea taarifa ya Wilaya, kuongea na watumishi wa Umma, atakagua mradi wa maji Minjingu, atakagua Kiwanda cha mbolea Minjingu, ataweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa daraja la Bonga –Endanachani na kuongea na wananchi katika uwanja waq michezo wa Kwaraa.
Tarehe 20 Waziri MKuu atafanya majumuisho ya siku sita ya ziar4a yake Mkoani Manyara katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ambapo Mkuu wa Mkoa huyo aliwataka wakazi wa mkoa huo kujitokeza kwa wingi kumpokea kwa kuwa kiongozi wa kitaifa husaidia kushauri na kusukuma maendeleo ya Mkoa .
Post a Comment
karibu kwa maoni