Matumaini ya klabu ya Arsenal kutwaa ubingwa wa England yanaanza kufifia baada ya kuchapwa na Watford 2-1 na hii ni Emirates.
Mlinzi
wa zamani wa Tottenham Younes Kaboul alianza kuiandikia Watford goli la
kwanza dakika ya 10 baada ya kuachia shuti kali lililomgonga Aaron
Ramsey na kutinga nyavuni.Dakika mbili na sekunde 57 baadaye Troy Deeney akaiandikia goli la pili Wtaford baada ya mpira uliopigwa na Etienne Capoue kupanguliwa na mlinda mlango Petr Cech na kisha kumkuta Troy aliyeandika bao safi.
Kipindi cha pili Arsenal walianza kwa kasi na kujipatia goli la kufutia machozi kutoka kwa Alex Iwobi baada ya kupanda pande safi lililochongwa na Alexis Sanchez.
Kwa mara ya mwisho Arsenal kushinda kikombe cha ligi kuu England ilikuwa msimu wa mwaka 2003-04 na kwa sasa wapo nyuma kwa alama tisa dhidi ya vinara Chelsea ambao wametoka suluhu ya 1-1 dhidi ya Liverpool.
Post a Comment
karibu kwa maoni