Kocha Msaidizi wa Azam FC, Idd Nassor Cheche, ametema cheche baada ya kusema itakuwa vizuri sana kama Shirikisho la Soka Afrika (Caf) litawapa wacheze na Yanga kwenye mchezo wa kusaka nafasi ya kutinga makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga inayoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika, inaweza kuangukia Kombe la Shirikisho endapo itaondolewa na Zanaco kwenye mchezo wao wa marudiano utakaopigwa wikiendi hii jijini Lusaka, Zambia baada ya hapa nyumbani kutoka sare ya bao 1-1.
Azam ambayo iliifunga Mbabane Swallows bao 1-0 kwenye mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho, imejipa matumaini makubwa ya kusonga mbele kutokana na ushindi huo wa nyumbani.
Kwa mujibu wa ratiba ya Caf, timu 16 zitakazoondolewa kwenye hatua ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika, zitaungana na 16 zilizofuzu Kombe la Shirikisho kusaka timu 16 zitakazocheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.
Cheche amesema: “Kwa kifupi huwa tunajiandaa kupambana na timu ya aina yoyote ile, lakini pale inapotokea unakutana na mpinzani wako mzuri zaidi yako ndiyo kinakuwa kipimo sahihi kwenu kujua kiwango chenu kipo levo gani.
”Yeyote atakayekuja mbele yetu tutapambana naye na tutahakikisha tunasonga mbele kwani malengo yetu ni kufika mbali zaidi ya hapa tulipo sasa,” alisema Cheche.
Post a Comment
karibu kwa maoni