Chelsea wakicheza ugenini wamechukua ubingwa wa Ligi Kuu ya England baada ya kupata ushindi wa 0-1 dhidi ya West Brom.
Goli pekee lililoipa ushindi Chelsea lilifungwa na Michy Batshuayi katika dakika ya 82.

Huu ni ubingwa wa mara ya tano wa EPL kwa Chelsea.
Tottenham ambao ndio waliokuwa wapinzani wa karibu wa Chelsea katika nafasi ya pili, walipoteza mchezo wao dhidi ya West Ham Mei 5, na hivyo kuifanya Chelsea kuhitaji kushinda mechi mbili kati ya nne zilizosalia.
Walishinda mechi yao dhidi ya Middlesbrough 3-0 Jumatatu Mei 8, na kukamilisha pointi walizohitaji kuchukua ubingwa kwa kuizaba West Brom siku ya Ijumaa Mei 12.SASA ANGALIA FURAHA MPAKA KUVUA NGUO HAHAAAAA HAAAAA
Chelsea wamefunga Wes Brom kwa bao 1-0 na kujihakikishia kubeba ubingwa wa Ligi Kuu England licha ya kubaki na mechi mbili mkonon.
Furaha ya wachezaji wa Chelsea ilianzia uwanjani hadi vyumbani na mshambuliaji nyota wa Chelsea, Diego Costa yeye alijiachia kabisa kwa kubaki na nguo ya ndani.
Post a Comment
karibu kwa maoni