0

Image result for MAGUNIA YA BANGI

Tume ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya kwa kushirikiana na kikosi maalumu cha jeshi la polisi wamekamata na kuteketeza magunia zaidi ya 400 ya bangi katika  kijiji cha Engalaoni wilayani Arumeru mkoani Arusha.
Kamishna wa Intelijensia wa mamlaka  ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya nchini, Bw Fred Kibuta amesema magunia hayo yalikuwa yamefichwa kwenye nyumba katika kijiji hicho ambacho wakazi wake wametelekeza nyumba zao na kukimbilia porini kukwepa kukamatwa
Naye Kamishna wa Oparesheni ya kudhibiti dawa za kulevya nchini, Mihayo Msikela amesema baadhi ya viongozi wa eneo hilo wanahusika katika ulimaji na uuzaji wa bangi, jambo ambalo linahitaji ushirikiano mkubwa toka kwa wananchi ili kudhibiti.
Arumeru ni miongoni mwa wilaya zinazosifika kwa ulimaji wa zao haramu la bangi ambapo hivi karibuni tume hiyo ilikamata magunia mengine 168  pamoja na watuhumiwa 19 Katika kijiji cha Losinoni kitongoji cha Engedeko.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top