0


MSHAMBULIAJI
Wayne Rooney amekuwa na mwanzo mzuri akiichezea kwa mara ya kwanza
klabu yake, Everton baada ya kufunga katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Gor
Mahia ya Kenya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam maarufu kama Kwa Mchina.


Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31, alifunga bao zuri kwa shuti la umbali wa mita 30 dakika ya 34.

Mchezaji
huyo aliyerejea Everton wiki iliyopita baada ya miaka 13 tangu ahamie
Manchester United amekumbushia kitu alichofanya wakati anajiunga na timu
hiyo ya Merseyside kwa mara ya kwanza kabisa alipofunga bao lake la
kwanza katika mechi ya kwanza dhidi ya Arsenal mwaka 2002, siku tano
kabla hajatimiza miaka 17.


Rooney alipata mpira akiwa umbali wa mita 40, akauvuta mbele kidogo kabla ya kufumua shuti lililotinga nyavuni.

Hata
hivyo, Gor Mahia wakasawazisha bao hilo kabla ya mapumzkiko kupitia kwa
mshambuliaji wa zamani wa Rwanda, mzaliwa wa Uganda, Meddie Kagere.


Kipindi
cha pili makocha wote, Dylan Kerr wa Gor Mahia na Ronald Koeman wa
Everton wakabadilisha vikosi vyao vyote, lakini bahati ilikwenda kwa
timu ya Ligi Kuu ya England, The Toffees waliopata bao la ushindi
kupitia kwa Kieran Dowell.


Gor
Mahia ilipata nafasi ya kucheza na Everton baada ya kuibuka bingwa wa
michuano ya SportPesa Super Cup, ikiwafunga mahasimu, AFC Leopatrds 3-0.


Timu
nane zilishiriki michuano hiyo ya wiki moja Uwanja wa Uhuru, Dar es
Salaam – mbali na Gor na Leopards, nyingine ni Tusker na Nakuru All
Stars za Kenya pia, Jang’ombe Boys ya Zanzibar, Simba, Yanga na Singida
Unted za Tanzania.


Wenyeji
Simba na Yanga hawakufika mbali kwa sababu wiki ya michuano hiyo
wachezaji wao wengi nyota walikuwa kwenye vikosi mbalimbali vya timu za
taifa na kujikuta wakitumia wachezaji wengi wa akiba na wa timu za
vijana.  


Vikosi vya leo vilikuwa; 

Gor
Mahia kipindi cha kwanza; Boniface Oluoch, Godfrey Walusimbi, Musa
Mohammed, Haron Shakava, Karim Niziyimana, Ernest Wendo, Kenneth Muguna,
George Odhiambo, Meddie Kagere, Jacques Tuyisenge na Boniface Omondi.


Kipindi
cha pili: Peter Odhiambo, Innocent Wafula, Mike Simiyu, Wellington
Ochieng, Joachim Oluoch, Philemon Otieno, Francis Kahata, Jean Baptiste,
Oliver Maloba, Jeconia Uyoga na Timothy Otieno.


Everton
FC kipindi cha kwanza; Stekelenburg; Connolly, Jagielka, Kenny,
Williams; Schneiderlin, McCarthy, Lennon, Klaassen, Lookman na Rooney.


Kipindi  cha pili: Hewelt, Baines, Keane, Davies, Mirallas, Pennington, Calvert-Lewin, Gueye, Barry, Besic na Dowell.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top