0


Rais Dk John Pombe Magufuli akizindua jiwe la msingi linaloashiria kuanza rasmi kwa mradi huo mkubwa kabisa utakaomaliza tatizo la maji katika mji huo. 
RAIS Dk John Pombe Magufuli anaendelea kutekeleza kwa kasi ahadi zake alizowaahidi wananchi wa Tanzania wakati akiwaomba kura wakati wa kampeni mwaka 2015.
Katika mkoa wa Kigoma moja ya ahadi zake kwa wananchi wa Mji mdogo wa Nguruka wilayani Uvinza, Rais Magufuli aliwaahidi wananchi hao kuwa ataitatua shida ya maji ya muda mrefu inayowakabili.
Rais Magufuli aliwahakikishia wananchi hao kuwa kupitia mto Malagarasi ambao ni jirani tu na mji huo (Kilomita 18 kutoka mji wa Nguruka) atawajengea mradi mkubwa wa maji ambayo yatatumika katika Wilaya yote ya Uvinza na maeneo jirani.
Hatimaye leo Rais Magufuli ameitekeleza ahadi yake na kuweka jiwe la msingi la mradi huo mkubwa kabisa katika miradi iliyopo mkoani Kigoma. Kwamujibu wa Rais Magufuli mradi huo utakamilika Desemba 31, 2017 na kuanza kuwahudumia wananchi ambao wana hamu kubwa ya kuona mradi huo ukianza kuwapatia maji.
Hizi ni juhudi za Rais za kuhakikisha kuwa wananchi wa Tanzania wanafaidika na rasilimali za nchi yao ambapo amefanikiwa kulinda rasilimali za nchi na kupambana bila kuchoka na wabadhirifu wa mali za umma, wala rushwa na mafisadi.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top